Sura mpya za maandamano - Wanamapinduzi wa Kenya wa Gen Z wanaopinga kodi - BBC News Swahili (2024)

Na Wycliffe Muia

BBC News, Nairobi

Sura mpya za maandamano - Wanamapinduzi wa Kenya wa Gen Z wanaopinga kodi - BBC News Swahili (1)

Chanzo cha picha, Reuters

Kizazi kipya cha waandamanaji wachanga wa Kenya kimeibuka barabarani na kulazimisha serikali kubadilisha baadhi ya mapendekezo ya kodi ambayo hayakuwapendeza watu wengi nchini humo.

Kilichoanza kama hasira katika TikTok kuhusu mswada wenye utata wa fedha kimebadilika na kuwa uasi - bila kupangwa na vyama vya siasa.

Serikali ya Rais William Ruto imeweza kufanya kile ambacho vizazi vya wanasiasa katika taifa hilo la Afrika Mashariki vimeshindwa kufanya - kuunganisha idadi kubwa ya Wakenya bila kutumia ukabila au vyama .

Siku ya Jumanne, mamia ya waandamanaji ambao wanahisi Wakenya tayari wametozwa ushuru kupita kiasi bila ya kuwa na ufanisi unaooneysha jinsi kodi yao inavyotumika , walistahimili makali vitoa machozi na mapambanano na polisi kuandamana katika mji mkuu, Nairobi, na kusababisha shughuli katikati mwa jiji kuvurugwa.

Wakiwa na simu zao za mkononi, walipeperusha moja kwa moja makabiliano makali na maafisa wa polisi.

Sura mpya za maandamano - Wanamapinduzi wa Kenya wa Gen Z wanaopinga kodi - BBC News Swahili (2)

Chanzo cha picha, EPA

Maandamano hayo yaliyopewa jina la "kuchukua bunge" yaliratibiwa na kuhamasishwa kwenye mitandao ya kijamii tofauti na yale yaliyokuwa yakiongozwa na kufadhiliwa na wanasiasa.

Waandalizi waliwahimiza waandamanaji wenzao kuvaa nguo nyeusi, lakini wengine bado walijitokeza wakiwa wamevalia jeans zilizochanika na nywele maridadi.

Waandamanaji vijana, maarufu kama Gen Zs - kwa kurejelea neno linalotumiwa kwa ujumla kuwaelezea wale waliozaliwa mwishoni mwa miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000 - walijitokeza kwa wingi, wakiapa kuhakikisha kwamba kutoridhika kwao hakuishii kwa alama ya reli tu au vibonzo vya kejeli mtandaoni.

“Sisi ni Gen Z, tuliweza kujipanga. Tunatumia TikTok kama kifaacha kuweza sio tu kuwahamaisha vijana kuja kuandamana bali kuwaelimisha ni kwa nini tunafanya hivyo,” mwandamanaji Zaha Indimuli aliwaambia waandishi wa habari.

Wengi wao walikuwa wakiandamana kwa mara ya kwanza na kutikisa mabango yenye maneno kama vile "Usilazimishe Ushuru" , huku wengine wakiimba: "Ruto lazima aondoke".

"Niko hapa nikitumikia nchi ninayoipenda. Ni mara ya kwanza ninafanya hivi kwa sababu wazazi wangu ni wazee na hawawezi kufanya hivyo tena," Ken Makilya, mwanafunzi wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 24, aliiambia BBC.

Unaweza Pia Kusoma
  • Muswada wa Fedha Kenya: Serikali yaondoa mapendekezo ya ushuru kwa bidhaa muhimu

  • William Ruto: Rais 'mtoza ushuru' anayezua hasira za Wakenya

  • Kwanini rais wa Kenya anataka wananchi wampende mtoza ushuru

Sura mpya za maandamano - Wanamapinduzi wa Kenya wa Gen Z wanaopinga kodi - BBC News Swahili (3)

Chanzo cha picha, AFP

Alama ya za reli (Hashtag) zilizotumiwa kuwashinikiza wabunge na kuwahimiza waandamanaji ni "#OccupyBunge" na "#RejectFinanceBill2024".

“Haya ndio maanadamano yangu ya kwanza. Natumai yatakuwa ya mwisho. Natumai mambo yatabadilika baada ya hili,” alisema Naserian Kasura, ambaye alipinga pendekezo la kutozwa ushuru vitambaa vya hedhi.

Juhudi za waandamanaji hao kuandamana hadi bungeni zilizimwa huku polisi wakitumia maji ya kuwasha kuwazuia.

"Tumekamatwa lakini msiwaruhusu wawafikie tafadhali endeleeni hadi bungeni," Hanifa Farsafi, anayeripotiwa kuwa mmoja wa waandalizi, alichapisha kwenye X, zamani Twitter.

Zaidi ya vijana 200 waandamanaji walikamatwa lakini baadhi yao waliachiliwa baada ya mawakili kwenda katika vituo vya polisi walimokuwa wamezuiliwa.

“Siendi, sishirikiani, kwanini unanikamata?” muandamanaji mmoja alisikika akisema kwenye video ya mtandaoni huku akikataa kupanda gari la polisi.

Sura mpya za maandamano - Wanamapinduzi wa Kenya wa Gen Z wanaopinga kodi - BBC News Swahili (4)

Chanzo cha picha, Reuters

Wale ambao hawakufanikiwa kufika mitaani kuandamana walisaidia kueneza habari hiyo kwa kutuma ujumbe, picha na video kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa vile maandamano hayo yalikosa uongozi wa wazi, polisi wamepata ugumu wa kuwalenga waandalizi na viongozi wa maandamano. Walipiga maruf*cku maandamano hayo ingawa waandamanaji walisema mahitaji yote yametimizwa.

Na tofauti na maandamano ya awali ya kisiasa dhidi ya serikali, hayakuwa na visa vya uporaji, uharibifu wa mali na kurusha mawe.

Hakuna misimamo ya kisiasa au miungano ya kikabila iliyotajwa - ni uamuzi wa wazi wa waandamanaji kusikilizwa.

Saa kadhaa baada ya waandamanaji kukusanyika , ofisi ya rais ilionekana kuitikia shinikizo na kutangaza kuwa itafutilia mbali baadhi ya vifungu vyenye utata vya muswada huo, ikiwa ni pamoja na pendekezo la asilimia 16 ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye mkate.

"Tumesikiliza maoni ya Wakenya," Kuria Kimani, mwenyekiti wa kamati ya fedha ya bunge, alisema katika kikao na wanahabari kilichohudhuriwa na Rais Ruto na wabunge katika muungano unaotawala.

Mabadiliko katika mswada wa fedha yalichochewa na "haja ya kuwalinda Wakenya dhidi ya kuongezeka kwa gharama ya maisha", Bw Kimani aliongeza.

Awali serikali ilikuwa imetetea ongezeko la ushuru, ambalo lilitarajiwa kuongeza $2.7bn (£2.1bn), ikisema kuwa zilihitajika kupunguza utegemezi wa mikopo kutoka nje.

Ushuru mwingine uliopendekezwa ambao umeondolewa ni pamoja na wa mafuta ya kupikia, huduma za pesa kwa simu na magari, ambayo wakosoaji walisema yangeathiri sekta ya bima.

Wabunge sasa wanajadili mswada huo uliorekebishwa na wanatarajiwa kuupigia kura Jumanne ijayo.

Upinzani ambao haukushiriki katika maandamano hayo, unataka kukataliwa kabisa kwa mswada mzima, ukitaja kuwa ni "adhabu".

Sura mpya za maandamano - Wanamapinduzi wa Kenya wa Gen Z wanaopinga kodi - BBC News Swahili (5)

Chanzo cha picha, EPA

Hashtag nyingine inayotumiwa na wanakampeni ni "#unfollowRuto", inayohimiza watu kukoma kumfuata rais kwenye X kwa nia ya ku*mshinikiza aondoe mswada huo.

Wameapa kuendelea na maandamano jijini Nairobi na miji mingine hadi mswada huo utakapotupiliwa mbali kabisa

Siku chache zilizopita, mshauri wa rais David Ndii alikuwa amepuuzilia mbali juhudi za mtandaoni zilizoanza kwenye TikTok takriban wiki mbili zilizopita, lakini kufuatia onyesho la nguvu la Jumanne alikubali mafanikio yao .

Kufuatia kuchapishwa kwa rasimu ya mswada huo, Wanatiktok walianza kutengeneza vielezi vya video ambavyo vilishirikiwa sana kwenye majukwaa mengine kama vile WhatsApp, Facebook, Instagram na X - ambayo yalivuma kwa siku kadhaa kusaidiwa na misukumo kutoka kwa washawishi mitandaoni nchini Kenya.

Mbinu moja ambayo imewalazimu wabunge kuchukua tahadhari ni orodha ya nambari zao za simu ambazo zimesambazwa kwenye mitandao ya kijamii zenye ujumbe "SMS Mbunge wako".

Mbunge Stephen Mule aliambia vyombo vya habari kuwa simu yake ilisakamwa na zaidi ya jumbe 30,000 kutoka kwa vijana wa Kenya wakimtaka kukataa mswada huo. Wabunge wengine pia wamelalamika kwamba simu zao zimekuwa hazitumiki kwa sababu ya idadi ya jumbe wanazotumiwa.

Vyombo vya habari vya ndani pia vimeyaangazia matukio hayo ya mtandaoni, na kuongeza sauti za maandamano na masuala kuhusu gharama ya maisha.

Baadhi walimtaka kiongozi mkongwe wa upinzani Raila Odinga, ambaye amekuwa akiongoza maandamano dhidi ya serikali kwa miaka mingi , kujiepusha na maandamano ya Jumanne.

Alikubali, na akichapisha kwenye mitandao ya kijamii : "Mimi ni baba mwenye fahari sana leo! Hongera kwa wale wote ambao kwa ujasiri walisimama kutetea haki zao!"

Sura mpya za maandamano - Wanamapinduzi wa Kenya wa Gen Z wanaopinga kodi - BBC News Swahili (6)

Chanzo cha picha, AFP

Mutuma Mathiu, mwanahabari mkongwe, alisema matukio ya Jumanne yamebadilisha mienendo ya siasa za Kenya : "Siasa za maandamano zilipata fursa mpya na kizazi kipya na tofauti cha Wakenya kilipata sauti yao kubwa."

Mchambuzi maarufu wa kisiasa Pauline Njoroge alikubali : "Sio tu wajasiri, pia ni watu waungwana sana na wanazungumza vizuri. Maandamano ya leo yanayoongozwa na vijana yamekuwa ya amani zaidi lakini pia yenye mafanikio makubwa."

Prof Kivutha Kibwana, msomi wa sheria na gavana wa zamani wa kaunti, alihimiza mazungumzo katika chapisho lake kwenye X : "Jambo hatari zaidi kwa serikali ni kutangaza vita dhidi ya vijana wake."

Dkt Willy Mutunga, jaji mkuu wa zamani, alisema vijana kote ulimwenguni walikuwa na adui mmoja - "Watawala katika nchi zao : "Maasi yanakaribia."

Serikali kwa muda mrefu imekuwa na hofu kwamba mitandao ya kijamii inaweza kutumika kuzua mifarakano na imeshinikiza uangalizi mkali zaidi na udhibiti.

Kundi la mtandaoni linalojulikana kama Wakenya kwenye X (XOT) linajulikana kwa kutoa wito kwa masuala muhimu ya kitaifa na Kenya ni miongoni mwa nchi zilizo na kiwango cha juu zaidi cha matumizi ya TikTok duniani kote .

Mnamo Machi, waziri wa mambo ya ndani alitishia kuzuia matumizi ya TikTok, ambayo alishutumu kwa kueneza maudhui mabaya.

Lakini waandamanaji hawana nia ya kulegeza kamba .

"Hatuogopi, hatujaguswa na huu ni mwanzo tu wa mapinduzi. Tunakuja, tuko wengi na kwa idadi ya kutosha," alisema Bi Indimuli pembezoni mwa maandamano ya Jumanne.

Unaweza Pia Kusoma
  • Muswada wa Fedha Kenya: Serikali yaondoa mapendekezo ya ushuru kwa bidhaa muhimu

  • William Ruto: Rais 'mtoza ushuru' anayezua hasira za Wakenya

  • Kwanini rais wa Kenya anataka wananchi wampende mtoza ushuru

Imetafsiriwa na Yusuf Jumah

Sura  mpya za maandamano - Wanamapinduzi wa Kenya wa Gen Z wanaopinga kodi - BBC News Swahili (2024)

References

Top Articles
Latest Posts
Article information

Author: Maia Crooks Jr

Last Updated:

Views: 6620

Rating: 4.2 / 5 (63 voted)

Reviews: 94% of readers found this page helpful

Author information

Name: Maia Crooks Jr

Birthday: 1997-09-21

Address: 93119 Joseph Street, Peggyfurt, NC 11582

Phone: +2983088926881

Job: Principal Design Liaison

Hobby: Web surfing, Skiing, role-playing games, Sketching, Polo, Sewing, Genealogy

Introduction: My name is Maia Crooks Jr, I am a homely, joyous, shiny, successful, hilarious, thoughtful, joyous person who loves writing and wants to share my knowledge and understanding with you.